KIKOSI cha Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Julai 08 2025 kiliingia kambini Dar es Salaam kisha alfajiri ya kuamkia Julai 9 kimekwea pipa kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi ya wiki tatu.
Hivyo kuelekea CHAN mambo ni moto na maandalizi yanaendelea kwa kasi ikiwa ni mwendelezo wa ukarabati wa Uwanja wa Mkapa ambao upo tayari kwa asilimia kubwa kuelekea CHAN.
Stars Agosti 02, 2025 itacheza mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Chan 2024 dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni Aishi Manula, Mohamed Hussen Zimbwe, Dickson Job.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Serikali wamebainisha kuwa kwa kiasi kikubwa maandalizi yanakwenda vizuri kwa ajili ya mashindano hayo ya Chan.
The post KUELEKEA CHAN…..TAIFA STARS YAKIMBILIA MISRI ‘KUVUNJA NAZI’…. appeared first on Soka La Bongo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!