DKT. BITEKO: UWEPO WA SGR UNAASHIRIA UTOSHELEVU WA UMEME NCHINI 

  • 4
Scroll Down To Discover

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema safari za treni za Reli ya Kisasa (SGR) zinazotumia umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.

Dkt. Biteko ameyasema hayo baada ya kuwasili Jijini Dodoma akitokea Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa treni ya umeme (SGR) kwa mara ya kwanza.

“Safari za treni ya umeme ya SGR ni ushahidi mwingine kuwa nchi ya Tanzania ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, viwanda mbalimbali vinajengwa na kongani za viwanda kuongezaka”, amesema Dkt. Biteko

Katika kuhakikisha umeme unatosheleza Dkt. Biteko amesema Wizara ya Nishati kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwepo wa kutosha wakati wote na kuongeza kuwa wizara inasimamia ujenzi wa laini nyingine ya kuutoa umeme kutoka Chalinze kwenda Dodoma kwa laini kubwa zaidi na kutoa umeme kutoka Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kwenda Dodoma baadae Singida, arusha hadi Mwanza.



Prev Post MHE. MWIGULU: SERIKALI ITAENDELEA KUIPA KIPAUMBELE TMA.
Next Post WIZARA YA HABARI IKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI SEKTA YA MAWASILIANO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook