Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Wachunguza Tukio la Utekaji na Urejeo wa Mwanamke Bahari Beach

  • 42
Scroll Down To Discover

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeeleza kuwa limepokea taarifa za kutekwa na kurejeshwa kwa mwanamke aliyejitambulika kwa jina la Christina Hezroni Polepole Kinyangazi, mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Bahari Beach, Mtaa wa Kitumba, Kinondoni.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilianza kuripotiwa kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 17, 2025, ambapo mtu aliyejitambulisha kwa jina la Humphrey Polepole alidai kuwa dada yake alichukuliwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumba yake kwa kuruka ukuta.

Jeshi hilo limethibitisha kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya usalama, huku likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za uchunguzi zikiendelea.



Prev Post Trump Afanyiwa Uchunguzi wa Kiafya, Adhibitika Kuwa na Tatizo la Mishipa ya Damu
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 19, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook