Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Sakata la Rasilimali za CHADEMA: Mawakili Wadai Msajili Amepotosha Hukumu

  • 35
Scroll Down To Discover

Mawakili wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho wamepinga vikali ‘uhalali’ wa barua iliyoandikwa na Msajili wa Mahakama ya Tanzania kwenda kwa Mawakili wa Saidi Issa Mohamedi, na wenzake wawili inayolenga kufafanua kuhusiana na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu kuhusiana na marufuku ya matumizi ya rasilimali za chama.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Julai 19.2025 Wakili Hekima Mwasipu amesema Mawakili watatu wanaoiwakilisha CHADEMA katika kesi hiyo ambao ni Hekima Mwasipu, Dkt. Rugemeleza Nshala na Mpale Mpoki walipigiwa simu na Naibu Msajili wa Mahakama wakielezwa kuwa wanapaswa kutuma anuani zao ili watumiwe barua kutoka kwa Msajili wa Mahakama, na walipofanya hivyo walipokea nakala ya barua (kupitia email) inayoeleza ufafanuzi wa uamuzi huo, ambapo barua hiyo ilionesha orodha ya watu 10 waliopigwa marufuku kujishughulisha na shughuli zozote za chama kwa namna moja au nyingine.

Kupitia taarifa yake kwa wanahabari, Wakili Mwasipu anasema barua hiyo ni batili na kwamba inakiuka msingi wa uamuzi huo, kwani uamuzi wa marufuku hiyo unawahusu Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambao hawapaswi kutumia raslimali za chama na kujishughulisha na shughuli za chama kwa namna yoyote ile, lakini wengine wote wamepigwa marufuku kutumia raslimali za chama pekee, hivyo barua hiyo ni batili.

“Waliozuiliwa kutumia raslimali za chama ni Katibu Mkuu na Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambayo ndio inahodhi mali za chama, na watu wengine waliozuiliwa kutumia mali za chama ni wafanyakazi, Mawakala na mtu yeyote ambaye atafanya kazi kwa shughuli kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu” -Wakili Mwasipu

Amesema kitendo cha Msajili wa Mahakama kuorodhesha orodha ya watu 10 kwenye barua yake ni kinyume na amri ya Mahakama, jambo ambalo ametafsiri kuwa ni Msajili au Naibu Msajili wa Mahakama kupitia barua hiyo ametoa hukumu.

Wakili Mwasipu amesema kufuatia hilo na kupitia maelekezo ya wateja wao, wamemwandikia barua Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, ambapo kupitia barua hiyo wamemweleza mambo mawili, moja ni kwamba hana mamlaka ya kutafsiri au kutoa tafsiri ya hukumu



Prev Post Makalla: Uteuzi wa Wagombea CCM Kufanyika Mwisho wa Julai – Video
Next Post Umoja Wa Mataifa Wazidi Kuliamini Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania (JWTZ)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook