
Rais wa Marekani Donald Trump (79) amefanyiwa uchunguzi wa kiafya baada ya kubainika kuwa na uvimbe mdogo kwenye miguu yake, hali ambayo madaktari wake wameithibitisha kuwa ni matokeo ya chronic venous insufficiency, yaani kushindwa kwa mishipa ya damu kurudisha damu vizuri kuelekea kwenye moyo.
Taarifa hiyo imesomwa na msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, kupitia barua rasmi iliyotolewa na daktari wa rais, Kapteni Sean Barbabella.
Kwa mujibu wa daktari Barbabella, Trump alifanyiwa vipimo vya kina, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa Doppler wa mishipa ya miguu, ambao ulithibitisha kuwepo kwa hali hiyo isiyo ya hatari. Daktari huyo aliongeza kuwa ni jambo la kawaida kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 70.
“Hakuna dalili yoyote ya ugonjwa wa kuganda kwa damu kwenye mishipa mikubwa, wala maradhi ya moyo, figo, au ugonjwa mwingine wa mwilini,” amesema Kapteni Barbabella.
Daktari huyo amesema hali ya Trump inadhibitiwa vyema na haina athari kwa majukumu yake ya kila siku kama Rais wa Marekani.https://youtu.be/mhHAfPndYNE
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!