Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mchezaji wa Yanga Aziz Andabwile Awatoa Taarifa Kuhusu Sintofahamu Mitandaoni

  • 18
Scroll Down To Discover

Mchezaji wa Klabu ya Yanga SC, Aziz Andabwile ameweka wazi ukweli kuhusu taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zikimhusu yeye na Klabu hiyo.

Kupitia taarifa yake kwa umma, mchezaji huyo amesema kuwa bado ni mchezaji halali wa Yanga SC na kwamba haki zake zote za kimkataba tayari zimeshalipwa na Klabu.

“Mimi ni mchezaji wa Young Africans Sports Club na haki zangu za kimkataba tayari nilishalipwa,” amesema.

Aidha, amewaomba waandishi wa habari kuhakikisha wanakuwa na vyanzo sahihi vya taarifa kabla ya kuchapisha habari, ili kuepuka kuleta taharuki miongoni mwa wachezaji na ndani ya timu zao.

“Niwaombe ndugu waandishi wa Habari kuwa na vyanzo sahihi vya taarifa ili kutoleta taharuki kwa wachezaji kwenye timu zao,” ameongeza.

Mwisho, ameomba radhi kwa wote waliochanganyikiwa au kukwazika kutokana na sintofahamu iliyojitokeza mitandaoni, huku akisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuitumikia Klabu ya Yanga kwa uaminifu na kujituma.



Prev Post Maandamano ya Oktoba 29 Hayakuwa Halali, TPBA Yatamka
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook