Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Ukurasa Mpya wa Historia: Mhe. Shigongo Aapa Kulitumikia Taifa kwa Uzalendo na Uadilifu

  • 6
Scroll Down To Discover

Katika ukumbi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana taifa lilishuhudia tukio lenye thamani ya kipekee katika historia ya uongozi wa kisasa. Mbele ya Bunge Tukufu, Mhe. Eric James Shigongo aliapa kwa moyo wa uzalendo, uaminifu, na dhamira thabiti ya kulitumikia Taifa la Tanzania.

Kitabu cha Katiba mkononi na moyo uliojaa heshima kwa wananchi waliomwamini vilikuwa ishara tosha ya ujasiri, uwajibikaji na nia njema ya kulinda maslahi ya Watanzania wote. Sauti yake iliposikika akila kiapo, haikuwa sauti ya mtu mmoja, bali sauti ya maelfu ya wananchi wa Buchosa waliompa dhamana ya kuwawakilisha  sauti ya matumaini, maendeleo na mabadiliko chanya.

Mhe. Shigongo wakati akiwa katika kampeni zake aliahidi kuendeleza siasa za maendeleo zenye kuunganisha watu, huku akisisitiza umuhimu wa amani kama msingi wa mafanikio ya kizazi cha sasa na kijacho. Ni matumaini ya wengi kwamba uongozi wake utaendelea kuwa chachu ya mabadiliko na dira ya maendeleo ya kweli kwa wana Buchosa.



Prev Post Wabunge Walivyowasili Bungeni Kwa Kikao cha Pili cha Bunge la 13 leo
Next Post Wanawake Wengi Wapo Jela India Kisa Unga
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook