

Kesi ya Sylvia Bongo Ondimba na mwanawe Noureddin Bongo Valentin, mke na mtoto wa aliyekuwa rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba, imeanza Jumatatu katika mahakama maalum ya jinai jijini Libreville. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa muda wa wiki nzima.
Wawili hao, wanaoshtakiwa kwa kutoonekana mahakamani, ni miongoni mwa watu 13 wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ubadhirifu wa mali ya umma, utakatishaji wa fedha, rushwa, na kughushi nyaraka rasmi.
Sylvia na Noureddin walikamatwa baada ya mapinduzi ya Agosti 2023 yaliyomuondoa madarakani Rais Ali Bongo na kumaliza utawala wa familia ya Bongo uliodumu kwa miaka 55.
Walitumikia kizuizini kwa miezi 20 kabla ya kuachiwa huru mnamo Mei 2025, wakidai kuwa waliteswa wakati wa kifungo chao mjini Libreville.
Kwa sasa, wawili hao wako uhamishoni mjini London na wamekataa kufika mahakamani, wakisema kesi hiyo ni ya kisiasa na imepangwa kwa ajili ya maonyesho tu.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!